UZUNDUZI WA KAMPENI YA KITAIFA YA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA [MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN]-RUVUMA

THRDC Yashiriki Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Mkoani Ruvuma Uwanja wa Majimaji uliopo Songea.
Kampeni hiyo imezunduliwa siku ya Jumamosi Tarehe 22 Julai 2023 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango .
THRDC pamoja na wanachama wake kutoka Kusini Mashariki ikiwa ni pamoja na Ruvuma na Mtwara.
Katika hotuba yake, Dr. Mpango amesema Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inapaswa kuangazia changamoto zinazowagusa wananchi wa hadhi zote wakiwemo watu wenye ulemavu na wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia.
Amesema kumekuwepo na ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa chini ambapo takwimu za Januari - Disemba 2022 zinaonesha matukio ya ukatili yaliyokuwa mengi zaidi ni ubakaji
ambayo ni 6,335, ulawiti 1,555 na mimba za utoto 1,557. Ametoa wito kwa Kampeni hiyo kusaidia waathirika wa vitendo hivyo kupata haki zao pamoja na kuagiza vyombo vya dola kuendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watuhumiwa wote wa matukio hayo.
THRDC kupitia wanachama wake wanaendelea kutoa msaada wa kisheria na kutoa elimu kwa wananchi. Vilevile Wanachama wa Mtandao wamezindua Kitua cha Msaada wa Kisheria Kusini
Mashariki ili kuwasaidia wananchi wengi zaidi.
THRDC SONGEA.