MAFUNZO KWA JESHI LA POLISI TANZANIA JUU YA MICHAKATO YA UCHAGUZI NA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA

Mafunzo haya ya siku mbili (17-18 Oktoba 2024) yalifunguliwa rasmi na CP. Awadhi Juma Haji kwa niaba ya IGP Camillus Mongoso Wambura.

Katika hotuba yake, CP. Awadhi Juma Haji alimshkuru Afadhe IGP kwa  kuruhusu mafunzo hayo kwa makamanda wa polisi nchini. Pia alipongeza sana THRDC kwa kuendelea kujitolea katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini, na hata kuandaa mafunzo haya kipindi hiki muafaka cha kuelekea uchaguzi mdogo Novemba 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

CP. Awadhi Juma Haji alieleza makamanda kuwa jukumu la utekelezaji wa sheria (Law Enforcement) ni muhimu katika kudumisha haki za binadamu, hasa kwenye michakato ya kidemokrasia kama vile uchaguzi.

Mgeni rasmi aliwasihi makamanda wa polisi mikoa kuhakikisha kwamba maafisa, wakaguzi na askari waliopo kwenye himata zao wanaelewa wajibu wao kikamilifu. “Kuheshimu haki za binadamu hujenga imani kwa umma, jambo ambalo linaimarisha uhalali wa jeshi la polisi” Alisisitiza mgeni rasmi.

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
17 Oktoba 2024