Ziara iliyotembelea makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Dar es salaam kwa lengo la kufanya majadiliano na kuwasilisha ilani ya Uchaguzi ya AZAKi 2024-2029,

Leo 12.10.2024, Mratibu wa kitaifa (THRDC), wakili, Onesmo Olengueumwa, kwa kushirikiana na viongozi wa AZAKi na wataalamu ameongoza Ziara iliyotembelea makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Dar es salaam kwa lengo la kufanya majadiliano na kuwasilisha ilani ya Uchaguzi ya AZAKi 2024-2029,

Ugeni ulipokelewa na viongozi wa CCM Taifa na Mkoa wakiongozwa na Ndugu John Mongella, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu.

Mratibu wa Kitaifa THRDC, ameeleza yakua Ilani hii ya AZAKi ni nyenzo muhimu sana kwa viongozi wa kisiasa wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwakuwa Ilani hii imetokana na maoni ya jamii kubwa ya watanzania wenye mfumo unaojiratibu kupitia AZAKi

 Ameeleza Ilani hii imegusa hatua na jitihada zilizifanywa na serikali katika  utekelezaji wa Ilani ya AZAKi ya 2015/2019,

Pamoja na jitihada hizo zizolifanyika, Wakili Onesmo Olengurumwa ametoa rai juu ya viashiria  vinavyopelekea kudhoofika kwa jitihada hizo na kuwataka viongozi wajao kuweza kuzingatia yale ambayo yameibuliwa na jamii kama changamoto na mapendekezo kwa serikali ijayo.

Baadhi ya masuala ya msingi ambayo Mratibu ameangazia kutoka katika  Ilani ya AZAKi  ni pamoja na hitaji la KATIBA Mpya, ikiwa ni hitaji la  wananchi wote pamoja vyama vyote vya siasa ikiwemo chama tawala (CCM), Maendeleo Endelevu na uchumi jumuishi kwa Wananchi wote, Mikakati thabiti ya kukabiliana na mabaliko ya Tabia nchi, Usimamizi thabiti wa rasilimali za kitaifa, Lishe na usalama wa chakula, uboreshwaji wa huduma za kijamii( Elimu,Afya,Maji),  Tunu za Taifa na Haki za binadamu.

Aidha kwa upande wake, Ndugu John Mongella, ameeleza yakua, Chama cha Mapinduzi  Kimepokea Ilani hii kwa nia ya dhati ikiwa tayari  kinatambua yakua Ilani hiyo imebeba mambo ya msingi ambayo kama chama wako tayari kuyatumia kikamilifu.

Ameeleza yakua kama chama tawala kinatambua mchango mkubwa na nafasi ya AZAKi katika masuala ya kimaendeleo na kusema yakuwa kuna kila haja ya kuhakikisha kwamba  kunakuwa na uendelevu wa mashirikishano baina ya AZAKi na Vyama vya kisiasa katika Masuala ya maendeleo kwa kuzingatia  kanuni na sheria za nchi.

THRDC
12.10.2024

DAR ES SALAAM HQ.