MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA - ZANZIBAR YAITEMBELEA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA

Menejimenti ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - Zanzibar (THRDC Zanzibar) yaitembelea Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba. Kupitia hilo, Mratibu wa THRDC Zanzibar, Bw. Baitani Mujuni ameutambulisha Mtandao kwa upande wa Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Bw. Mujuni ameelezea kwa kina kazi zinazofanywa na Mtandao, ikiwemo mashirikiano mbalimbali kati ya Mtandao na mamlaka kama vile vyuo vya mafunzo, mahakama n.k.
Mtandao ulipata pia wasaa wa kutambulisha mashirika wanachama 34 waliopo Pemba.
Mhe. Salama Mbarouk Khatib ameukaribisha sana Mtandao, na kupongeza kazi zinazofanyika. Pia amehimiza haki za binadamu ziangaliwe kwa mapana na usawa zaidi katika jamii zetu, hasa Pemba. Mheshimiwa amegusia juu ya haki nyingi zinazovunjwa ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, na ameuhimiza Mtandao kupitia wanachama kuliangalia zaidi hilo. Mheshimiwa amekaribisha THRDC Zanzibar katika ofisi zake kwa ajili ya kuyajenga zaidi juu ya haki za binadamu kwa mkoa wa Kaskazini Pemba.
Pichani: Mhe.Salama Mbarouk Khatib, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba (katikati), Bw. Baitani Mujuni, Mratibu THRDC Zanzibar (kulia), na Bi. Shadida Omar Ali, Afisa Programu THRDC Zanzibar (kushoto).
Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - Zanzibar
31 Agosti 2023.