MIAKA 10 YA THRDC

"Shukrani kuona mmeitikia wito wetu kwa wingi, kweli inafurahisha nasema ahsante sana. Kwa niaba ya mtandao nawashukuru najua wengi mmetoka mbali na yote hii inaonyesha kudhihirisha utayari pamoja na mapenzi makubwa ya utetezi wa haki-M/kiti Bodi ya Wakurugenzi THRDC, Jaji Mstaafu, Joaquine Demello.


Kikubwa tulichokifanya miaka hii 10, tumehakikisha watetezi wa haki za binadamu wanashiriki mifumo ya ndani nan je ya haki za binadamu na juzi tulikuwa Geneva Uswisi na wizara ya katiba na sheria, kuhakikisha mapendekezo ya haki za binadamu yanakubaliwa na mwaka huu tumepata mapendekezpo mengi yaliyokubaliwa na Tanzania-Mratibu THRDC, @olengurumwa2


"Twendeni na "approach" kuwa tunataka kujenga nchi yetu. Twendeni na approach kuwa hakuna wa kujenga nchi yetu isipokuwa sisi.
Twendeni na approach ya kudumisha mila na desturi nzuri na kuacha zile mbaya. Hii nchi ni yetu." Rais Samia Suluhu Hassan


"Ibueni maovu yanayofanyika, njooni tukae tuzungumze, waziri yupo, vyombo vya usalama vipo. Mna tatizo mwambieni Waziri, ataitisha tutakaa kitako, tutazungumza."- Rais Samia Suluhu Hassan


"Tanzania tumekuwa mbele katika kukuza na kulinda haki za binadamu nchini kwetu. Dhana nzima ya watetezi wa haki za binadamu, mimi kama mwanadamu pia nakubaliana nayo. " Rais Samia Suluhu Hassan

"Hali ya watetezi wa haki za binadamu imekuwa ikiboreka, ikiendelea kuwa nzuri mwaka hadi mwaka. Pamoja na changamoto ambazo tumekuwa tukizipitia katika utendaji kazi wetu"-Mkuu wa Dawati la Utetezi THRDC, Wakili Leopold Mosha