MAFUNZO KWA MA AFISA WA MAGEREZA JUU YA MATUMIZI YA MUONGOZO WA MALALAMIKO NA MAWASILIANO KWA WANAFUNZI NA MAHABUSU ZANZIBAR.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - Zanzibar (THRDC Zanzibar), umeendelea kushirikiana na Chuo cha Mafunzo Zanzibar (ZIEO) katika matumizi ya muongozo wa utoaji malalamiko na mawasiliano kwa wanafunzi na mahabusu Zanzibar.Jumatatu ya tarehe 28 Agosti 2023, ZIEO imeongoza utoaji elimu kwa maafisa magereza mjini Pemba juu ya matumizi ya muongozo huo. Mchakato huu ni kwa nia ya kuimarisha ufanisi wa matumizi ya muongozo ulioundwa. Ikumbukwe ya kwamba, mchakato huu umefanywa na timu ya wadau wa haki za binadamu ambao ni ZIEO, THRDC, Mahakama kuu, Polisi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Zanzibar Child Right Forum (ZCRF), na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP Office).
Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - Zanzibar
(THRDC - Zanzibar)
29 Agosti 2023.