Shirika mwanachama la Agape Aids Control lapata msaada wa kuchimbiwa kisima, motor ya kisima hicho, na kufungiwa solar.
Msaada huu umetolewa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, chini ya Idara ya Maendeleo ya jamii, kwa ajili ya Kilimo cha Umwagiliaji katika Shamba lenye ukubwa wa takribani Ekari 5 ambalo linamilikiwa na shirika.
Kisima hicho kitasaidia upatikanaji wa maji wa wasichana waliokosa haki yao ya msingi ya kupata elimu kutokana na unyanyasaji wa kijinsia walioupitia.
Shirika la Agape linatoa shukrani za kipekee kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga.