THRDC YAPOKEA UGENI KUTOKA ZAFELA.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umepokea ugeni kutoka Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA). Ugeni huu umepokelewa leo Jumanne 1 Agosti 2023, katika ofisi za makao makuu ya Mtandao. Hii ni kwa nia ya kuboresha mashirikiano kati ya Mtandao na mwanachama wake wa Zanzibar, ikiwemo ZAFELA. Pichani kutoka kushoto ni Meneja Programu wa Mtandao Bw. Remmy Lema, Mkurugenzi wa ZAFELA Bi. Jamila Juma, na
Mtendaji wa ZAFELA Bi. Rufeya Hamis Juma.
Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)