JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI DARESALAAM

THRDC kupitia Mratibu taifa, Bw- Onesmo Olengurumwa ilipata fursa ya kufanya wasilisho juu ya
changamoto za kodi, na mapendekezo ya kuboresha sheria ya kodi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali. Mpaka sasa MTANDAO umeyafikia zaidi ya mashirika 1400 tangu Januari 2023 katika kutoa elimu hii na kujadiliana kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zilizopo. Pamoja na hayo MTANDAO umeendelea kupanua wigo wa majadiliano kuhusu usimamizi, uendeshaji wa mashirika, na sheria za kuzuia utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi.